Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sera za uhamiaji zimepitwa na wakati, tubadilike: IOM

Sera za uhamiaji zimepitwa na wakati, tubadilike: IOM

Leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kando ya mjadala wa wazi kutafanyika kikao cha ngazi ya juu kuhusu uhamiaji,  kikao kilichoitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Lengo la kikao hicho ni kuhamasisha ushirikiano na hatua za pamoja za kushughulikia matatizo na changamoto za uhamiaji wakati huu ambapo kuna mkanganyiko kuhusu uhamiaji, ukimbizi na wasaka hifadhi.

Kuwezesha uhamaji salama wa binadamu ni mojawapo ni mojawapo ya mipango ndani ya malengo ya maendeleo ya endelevu, SDGs, jambo ambalo linataka uratibu siyo tu baina ya nchi bali pia katika ngazi ya serikali na wadau wengine wakati huu dunia ikishuhudia janga la wakimbizi wanaotoka Afrika na Mashariki ya Kati kwenda Ulaya.

William Swing ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji ambapo alipohojiwa na Reem Abaza wa Radio ya Umoja wa Mataifa amesema kinachotokea sasa ni jamii ya kimataifa kushindwa kubadilika kutokana na hali ya sasa na hivyo..

(Sauti ya Swing)

“Natumai kutoka mkutano huu kutaibuka uelewa zaidi wa mazingira tunamoishi sasa kuwa uhamiaji umekuwa ndio mwelekeo wa zama za karne ya sasa, na sera zetu zimepitwa na wakati kwani haziendani na hali halisi ya kibinadamu.”