Msanii wa Nigeria, Nneka, atumia muziki kupigania usawa wa jinsia
Katika mfululizo wa Makala za Benki ya Dunia kuhusu muziki kwa ajili ya maendeleo, tunakutana na nyota wa Nigeria, Nneka, ambaye ana uraia wa Nigeria na Ujerumani. Nneka, kama wanamuziki wenzake kutoka barani Afrika, wamejiunga katika mchakato wa Benki ya Dunia wa kutumia muziki kuchagiza mabadiliko na kuleta maendeleo.
Katika Makala hii, Joshua Mmali anatumegea kidogo kuhusu ushiriki wa Nneka katika mchakato huu.