Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto nchini Kiribati kuanza kupatiwa chanjo dhidi ya kuharisha

Watoto nchini Kiribati kuanza kupatiwa chanjo dhidi ya kuharisha

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema watoto visiwani Kiribati watanusurika dhidi ya ugonjwa wa kuharisha unaosababishwa na kirusi kiitwacho Rota baada ya taifa hilo kuwa la kwanza katika ukanda wa Pacific kupitisha chanjo dhidi ya kirusi kiitwacho Rota. Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(TAARIFA YA GRACE)

Kwa usaidizi kutoka UNICEF, wizara ya afya ya nchi hiyo imetangaza kuanza kwa chanjo hiyo leo ikiiwa ni sehemu ya mpango wa kunusuru watoto.

Kuanzia leo chanjo hiyo itakuwa ikitolewa ili kuwalinda watoto dhidi ya kuharisha kunakotishia uhai wao ambapo majimbo yote nchini Kiribati yatafikiwa. Katika muktadha huo Mkuu wa UNICEF katika ukanda wa Pacific Dr Karen Allen amesema kirusi hicho huathiri watoto takribani wote walioko chini ya umri wa miaka mitano na kwamba utolewaji wa chanjo utapunguza idadi ya watoto wanaokufa nchini humo kwa ugonjwa unaoweza kuzuilika.

Mpango huo umedhaminiwa na serikali ya New Zeleand na UNICEF Australia ambapo shirika hilo litatoa usaidizi wa kitaalamu na kifedha kwa serikali ya Kiribati kwa miaka mitatu ijayo pamoja na mpango wa lishe na huduma za kujisafi.