Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yafikisha misaada ya chakula Myanmar

WFP yafikisha misaada ya chakula Myanmar

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), limesema kuwa limefanikiwa kufikisha msaada wa chakula kwa wathiriwa 82,000 wa mafuriko nchini Myanmar tangu lilipoanza operesheni zake tarehe 2 Agosti. Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

WFP imesema hivi sasa inashirikiana na wadau wengine katika jitihada za kufikisha chakula kwa zaidi ya watu 200,000 walioathiriwa na mafuriko pamoja na maporomoko ya ardhi nchini humo.

Serikali ya Myanmar na kampuni za ndege nchini humo zimetoa ndege zao kusaidia WFP kufikisha chakula kwa waathiriwa.

Inakadiriwa kuwa robo milioni ya watu katika majimbo 12 yalkiwemo Bago, Chin, Kachin na Rakhine wanahitaji msaada wa dharua baada ya barabara kuharibiwa na mvua kubwa za Monsoon.