Wanahabari Zanzibar watakiwa kukuza demokrasia na amani
Umoja wa Mataifa nchini Tanzania umevitaka vyombo vya habari visiwani Zanzibar, kutumia nafasi yake kukuza demokarsia na amani wakati wa uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.
Mwakilishi mkazi wa UM nchini humo Alvaro Rodriguez amewaambia wanahabari katika mkutano na vyombo hivyo leo kuwa jukumu la kuhakikisha uchaguzi huru na wa amani sio wa tume ya uchaguzi na vyama vya siasa pekee na kutaka tasinia hiyo kuwa wajumbe wa amani na majadiliano.
Akizungumzia mafanikio ya Umoja wa Mataifa visiwani Zanzibar Rodriguez amesema mojawapo ni uwezeshaji wa wanawake kushika nyadhifa za kisiasa na kuanzishwa kwa redio za kijamaii zilizotumika kutoa elimu ya uraia pamoja na kuwa jukwaa la haki za wanawake na watoto.
Kwa upande wao waandishi wa habari wanazungumzia wajibu wao katika amani na demokarsia kulekea uchuguzi mkuu
(SAUTI)