Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nusu ya wanaojidunga madawa wanaugua hepatitis C:UNODC

Nusu ya wanaojidunga madawa wanaugua hepatitis C:UNODC

Mkurugenzi Mkuu  wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC Yury Fedotov amesema watu milioni 6.3 ambao ni sawa na nusu ya watu wanaojidunga madawa wanaishi na homa ya ini aina ya hepatitis C. Taarifa kamili na Priscilla Lecomte.

(TAARIFA YA PRSCILLA)

Wakati maadhimisho ya ugonjwa wa homa ya ini aina ya Hepatitis C ikiadhimishwa kesho kimataifa, UNODC inasema licha ya kwamba ugonjwa huo unazuilika  na kutibika lakini unasambaa na kusababisha vifo na madhila kwa mamiloni ya watu kote duniani.

Taarifa ya UNODC inamnukuu Mkuu wa shirika hilo akisema kuwa juhudi dhidi ya hepatitis C zinahusiana na HIV kwani magonjwa hayo yote huambukizwa kwa kupitia damu na kupitia udungwaji wa sindano usio salama.

Bwana Fedotov anasema ili kufanikisha malengo pacha ya kutokomeza HIV na Hepatitis C watu wanaojidunga madawa wanahitaji huduma za kinga, upimaji na matibabu lakini akasema kuwa mara nyingi upatikanaji wa huduma hizo ni finyu au hazipo kabisa hususani kwenye magereza  na mazingira kama hayo.

Akizungumza na idhaa hii, Daktari Janet Mgamba ambaye ni mkurugenzi msaidizi wa kitengo cha kudhibiti magonjwa ya milipuko nchini Tanzania anaeleza hali ilivyo na mikakati ya nchini hiyo.

(Sauti ya Dkt. Janet)