Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Syria ugenini wazidi Milioni Nne:UNHCR

Wakimbizi wa Syria ugenini wazidi Milioni Nne:UNHCR

Idadi ya raia wa Syria waliokimbia nchi yao ili kusaka hifadhi nchi jirani imeongezeka na kufikia zaidi ya Milioni Nne.Taarifa zaidi na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Hiyo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR ambapo Kamishna wake mkuu Antonio Guterres amesema ni janga kubwa kwa shirika hilo kukabiliana nalo katika kipindi cha miaka 25.

Bwana Amesema ongezeko hilo ni la kasi kubwa, kwa kuwa miezi kumi iliyopita idadi ilikuwa Milioni Tatu kando ya wananchi wengine Milioni Saba nukta Sita wa Syria ambao ni wakimbizi ndani ya nchi yao.

Amesema kinachohitajika sasa ni usaidizi kwani wanaishi katika mazingira duni huko ugenini ikiwemo Uturuki, Lebanon, Jordan na Iraq  huku ufukara ukiwanyemelea kila uchao.

Mara ya mwisho idadi ya wakimbizi kutoka nchi moja kuvuka Milioni nne ilikuwa mwaka 1992 ambapo wakimbizi kutoka Afghanistan walikuwa Milioni Nne nukta Sita.