Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna matumaini ya kuzalisha chakula kingi 2015 kuliko ilivyotarajiwa - FAO

Kuna matumaini ya kuzalisha chakula kingi 2015 kuliko ilivyotarajiwa - FAO

Shirika la Chakula na Kilimo, FAO, limesema kuwa hali nzuri ya ukulimwa wa nafaka itachangia uzalishaji wa kiwango ambacho hakikutarajiwa duniani mwaka huu, licha ya kuwepo wasiwasi kutokana na mvua za El Niño.

Hata hivyo, FAO imesema kuna wasiwasi kuhusu uzalishaji wa mahindi Kusini mwa Jangwa la Sahara, pamoja na uzalishaji duni wa chakula katika maeneo mengine ambayo mara kwa mara hayana uhakika wa chakula.

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya makadirio ya kila mwezi kuhusu bei ya chakula, uzalishaji wa nafaka kote duniani mwaka huu unatarajiwa kufika tani milioni 2,527, ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.1 chini ya rekodi iliyowekwa mnamo mwaka 2014, ingawa ni afadhali kuliko makadirio yaliyofanywa mwezi uliopita.