OPCW yakaribisha uteketezaji wa sialaha za kemikali

17 Juni 2015

Shirika la kupinga matumizi ya silaha za kemikali(OPCW) imekaribisha hitimisho la uteketezwaji wa silaha za kemikali kutoka Syria uliotekelezwa na meli ya Marekani ifahamikayo kwa jina Cape Ray.

Kwa mujibu wa OPCW mnamo June 11 na 12 timu kutoka shirika hilo ilishuhudia uteketezwaji wa tani kadhaa ambapo serikali ya Ujerumani , na Finland zimeshiriki katika kufanikisha zoezi hilo.

Akikaribisha hatua hiyo Mkurugenzi Mkuu wa OPCW Balozi Ahmet Üzümcü amesema hii ni hatua muhimu katika kuteketeza matumizi ya silaha za kemikali kutoka Syria na kusema kuwa mchakato mzima umefanyika kwa njia salama na kwa ufanisi na amewashukuru wadau walioshiriki katika mchakato huo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter