Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha mpango wa ujenzi wa Somalia

UM wakaribisha mpango wa ujenzi wa Somalia

Umoja wa Mataifa, Serikali ya Shirikisho la Somalia na wabia wafadhili wamekaribisha leo utiwaji saini wa mpango wa pamoja wa maendeleo na uwezeshaji wa ujenzi ambao unajikita katika maeneo sita (SDRF).

Taarifa ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kutoka nchini Somalia inasema kuwa mpango huo wa pamoja unachagiza ujenzi wa amani na ujenzi wa malengo ya taifa la Somalia pamoja na maono ya serikali ya nchi hiyo ya mwaka 2016 .

Mpango huo pia unajikita katika kufanikisha mchakato wa ujenzi wa taifa, upitiaji wa katiba, uchaguzi, utawala wa kisheria uwezeshaji vijana na uwezeshaji wa uwezo wa kitaasisi.

SDRF pia inatajwa kupigia chepuo ahadi ya jumuiya ya kimataifa na serikali ya Somalia kufanya kazi pamoja katika kuinua maisha ya raia wa nchi hiyo wakiwamo wanawake, wanaume na watoto.