Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila nishati endelevu hakuna maendeleo: Dk Kandeh

Bila nishati endelevu hakuna maendeleo: Dk Kandeh

Mkutano kuhusu nishati endelevu kwa wote umeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York ambapo wadau wa nishati kutoka nchi wanachama, mashirika ya kimataifa na asasi mbalimbali wanajadili  uwezekano wa upatikanaji wa nishati ya bei nafuu kwa wote. Taarifa kamili na Joseph Msami.

(TAARIFA YA MSAMI) 

Mkutano huo ulioanza hii leo utashuhudia majadiliano kutoka kwa mawaziri wa nishati kutoka mataifa mbalimbali duniani ambapo pia katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- Moon anatarajiwa kuhutubia.

Katika mahojiano na radio ya Umoja wa Mataifa msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu nishati endelevu Dk. Kandeh Yumkella amezungumzia umuhimu wa nishati kwa maendeleo akisema ni changamoto kubwa kwa watu wote duniani kupata nishati akisema wengi wasio na nishati ya umeme ndiyo maskini.

(SAUTI DK KANDEH)

Ili kutowesha umaskini utokanao na ukosefu wa nishati duniani tunahitaji uwekezaji zaidi na utashi wa kisiasa ili kuwavutia wawekezaji kuwezesha nishati duniani.

Amesema kote duniani watu bilioni moja na laki nne hawana nishati ya umeme na hivyo kukosa maji safi na kusalia masikini.