Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watalaam wa Umoja wa Mataifa waomba jamii ishirikishwe katika ajenda ya maendeleo ya baada ya 2015

Watalaam wa Umoja wa Mataifa waomba jamii ishirikishwe katika ajenda ya maendeleo ya baada ya 2015

Kundi la watalaam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamezisihi nchi wanachama kutambua na kuendeleza mchango wa jamii katika kuunda malengo ya maendeleo endelevu ya baada 2015.

Katika taarifa iliyotolewa leo wakati wawakilishi wa serikali wanakutana mjini New York kwa ajili ya kuunda mfumo wa ufuatiliaji na tathmini wa malengo ya maendeleo, watalaam wamezingatia umuhimu wa ushirikishwaji wa jamii.

Wamesema jamii inayochangamka na inayojieleza huru ni muhimu sana ili kusaidia serikali kubuni suluhu ya changamoto za maendeleo, na pia kuhakikisha sauti za watu wote zinasikika.

Watalaam hao wameonya kuhusu ongezeko la mashambulizi dhidi ya wadau wa jamii na wanaharakati wa jamii, na ongezeko pia la masharti dhidi ya uhuru wa kujieleza na kuandamana kwa amani.