Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajali za barabarani huua watoto 500 kila siku duniani:WHO

Ajali za barabarani huua watoto 500 kila siku duniani:WHO

Wakati wiki ya usalama barabarani ikianza leo, Shirika la Afya ulimwenguni, WHO limesema uhai wa watoto uko mashakani kila uchao kutokana na ajali za barabarani. Joseph Msami na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Joseph)

Ujumbe wa mwaka huu ukiwa watoto na usalama barabarani, WHO inasema ulimwenguni kote kila siku watoto 500 hufariki dunia ilhali wengine wengi hujeruhiwa kutokana na ajali za barabarani, huku ajali hizo zikiwa chanzo kikubwa cha vifo kwa vijana barubaru hususan wavulana.

Kwa mantiki hiyo WHO inataka kutumia fursa hii kuangazia madhila ya watoto barabarani na kuchukua hatua kuhakikisha usalama wao wakati huu bara la Afrika linachukua usukani kwenye vifo vya watoto barabarani katika nchi za vipato vya chini.

Ukanda wa Mediterania Mashariki ni wa pili ambapo WHO inasema vifo vya watoto kutokana na ajali za barabarani huibua changamoto kubwa bila kujali uwezo wa kipato kwa nchi husika.