Bodi ya kimataifa ya kudhibiti Mihadarati kufungua kikao chake cha 113 mjini Vienna( INCB)

4 Mei 2015

Kikao cha 113 cha bodi ya kimataifa ya kudhibiti mihadarati (INCB) kimeaanza Jumatatu tarehe 4 Mai na kitachagua rais mpya na ofisi zake miongoni mwa wajumbe wa bodi hiyo. Katika kikao hiki ambacho kinaendelea hadi Mai 15 , bodi itatathimini uzingatiaji wa mikataba mitatu ya kimataifa ya kudibiti dawa za kulevya au mihadarati katika nchi zaidi ya 200.

Akifungua kikao hicho kaimu rais, Werner Sipp, amemshukuru Rais wa zamani na mjumbe wabodi aliyestaafu Dr. Lochan Naidoo kwa uongozi wake na juhudi kubwa za kuweka masilahi ya walioathirika na mihadarati katika msitari wa mbele kila wakati.

Bwana Sipp amesema ari yake kama daktari akifanya kazi katika msitari wa mbele kwenye tiba na kuwasaidia vijana nchini kwake Afrika ya Kusini kurejea katika maisha ya kawaida na kuondokana na mihadarati imekuwa amana kubwa kwa bodi hiyo.

Mr. Sipp pia amekaribisha wajumbe wapya watatu wa bodi akisema kwa pamoja wataleta elimu na utaalamu katika Nyanja mbalimbali za kudhibiti mihadarati ikiwemo, magonjwa, utafiti, sheria, matibabu na ukarabati ambavyo vitasaidia uwezo wa bodi hiyo kufuatilia na kuchagiza utekelezaji wa mikataba na majadiliano na nchi wanachama.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter