Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Burundi iko njia panda : Mkuu wa haki za binadamu wa UM

Burundi iko njia panda : Mkuu wa haki za binadamu wa UM

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binaadamu Zeid Ra'ad al Hussein amehitimisha ziara yake ya siku nne nchini Burundi.

Baada ya kukutana na wadau mbalimbali za siasa za Burundi ameichagiza serikali ya nchi hiyo kuhakikisha inamaliza hujuma zote zinazofanywa na kundi la vijana kutoka chama tawala ili kuiweka nchi katika mazingira bora ya uchaguzi mwezi ujao. kutoka Bujumbura, muandishi wetu Ramadhani KIBUGA anasimulia zaidi..

(Taarifa ya Kibuga)

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Bujumbura mwishoni mwa ziara yake ya siku mbili nchini Burundi, Bwana Zeid ameeleza wasiwasi wake juu ya hali ya mvutano na ghasia inayoongezeka nchini humo wakati wa kuelekea uchaguzi wa mwezi Mei na Agosti mwaka huu.

Kamishna mkuu huyo wa haki za binadamu amesema mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari, viongozi wa kisiasa au familia zao, na harakati wa haki za binadamu ni dalili mbaya inayotishia watu wengi nchi humo na jamii ya kimataifa.

(Sauti ya Zeid)

“Baadhi ya watu wa hofu na tayari wamekimbia nchi hii kabla ya uchaguzi wa Rais mwezi Juni. Takribani watu elfu Sita yaamini wamesaka hifadhi Rwanda pekee. Idadi ya watu waliovuka mpaka siku mbili zilizopita imeongezeka na kuwa elfu Moja kwa siku. Wengi waliokimbia wameeleza umoja wa Mataifa sababu inayochochea ni vitendo vya hao wanamgambo.”

Hatimaye Bwana Zeid amekaribisha jitihada zilizofanyika katika maswala ya maridhiano baina ya makabila ya Burundi au usawa wa kijinsia akizingatia umuhimu wa kuongeza bidii ili kuondoa nchi hii kutoka kwa janga la umaskini.