Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Milioni 21 waacha shule Mashariki ya kati na Afrika : UNICEF

Milioni 21 waacha shule Mashariki ya kati na Afrika : UNICEF

Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto na lile la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO) kupitia taasisi yake ya takwimu inasema kuwa licha ya hatua kubwa katika kukuza uandikishaji wa watoto mashuleni katika muongo uliopita, mtoto mmoja kati ya wanne pamoja na barubaru zaidi ya milioni 21 huko mashariki ya kati na kaskazini mwa Afrika (MENA) ama hawako shuleni au katika hatari ya kuacha shule.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo aslimia 40 ya idadi ya waliojiandikisha shule katika ukadna wa MENA katika muongo uliopita ilitoa matumaini na fursa kwa mamilioni.

Hata hivyo maendeleo hayo yameshuka kwa sababu tofauti ikiwamo umasikini, ubaguzi, machafuko pamoja na kiwango hafifu cha kujifunza imesema ripoti hiyo.

UNICEF na UNESCO zimezitaka serikali za MENA kuzidisha juhudi zake katika kutoa kipaumbele katika mahitaji ya elimu kwa familia ambazo ziko hatarini kuikosa na zile ambazo hazinufaiki kwa elimu. Mashirika hayo yametaka kuwepo kwa sera mpya zinahitajika katika kukuza masomo ya chekechea, kukabiliana na wimbi la kuacha shule na ubaguzi wa kijinsia .