Skip to main content

Serikali mtuelewe Daadab isifungwe: UNHCR

Serikali mtuelewe Daadab isifungwe: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema tangazo la serikali ya Kenya kutoa muda wa miezi mitatu kuifunga kambi ya wakimbizi Daadab na kisha kuwarudisha makwao wakimbizi wa Somalia zaidi ya 350,000 limewastua , na kuitolea mwito serikali ya Kenya kutafakari upya.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii msemaji wa UNHCR nchini Kenya Emmanuel Nyabera amesema UNHCR imeanza mazungumzo na serikali ya Kenya ili kuangalia maeneo yanaoyoweza kufanyiwa kazi huku akikisistiza kuwa shirika hilo linatambua changamoto ya usalama inayolikumba taifa hilio kwa sasa.

Nyabera kwanza anaeleza mwitiko wa awali wa UNHCR baada ya tangazo la kuifunga kambi hiyo.