Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala la maendeleo na mizozo barani Afrika baadhi ya ajenda za wakuu wa AU

Suala la maendeleo na mizozo barani Afrika baadhi ya ajenda za wakuu wa AU

Kikao cha kawaida cha wakuu wa nchi wanachama wa Muungano wa Afrika kinaanza Alhamisi huko Addis Ababa, Ethiopia. Kikao hicho kinafanyika wakati Afrika ikiwa inagubikwa na mizozo kuanzia Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo  na Sudan Kusini. Je nini zitakuwa ajenda za kikao hicho? Assumpta Massoi wa Idhaa hii amefanya mahojiano kwa njia ya simu na mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi, ambaye yuko Addis Ababa alikohudhuria vikao tangulizi vya Mawaziri wa Mambo ya kigeni wa AU. Balozi Manongi anaanza kwa kuelezea ajenda kuu.