Ziarani, Mia Farrow asisitiza haja ya kusaidia watoto wa CAR
Mia Farrow, mcheza filamu maashuhuri, mwanaharakati na balozi mwema wa UNICEF amekamilisha ziara yake ya nne nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambko amejionea madhara ya ukatili uliokithiri, na pia kukutana na watu na kuwasikiliza wasimulia hadithi za ujasiri wa kutia moyo.
Akiwa mji wa Boda, yapata mwendo wa saa nne barabarani kutoka mji mkuu Bangui, Farrow alikutana na familia za Waislamu walionaswa kwenye eneo lililozingirwa na makundi hasimu yaliyojihami, na kusikia zikihadithia kuishi maisha ya kuogopa kuvamiwa kila uchao. Kwa mengi kuhusu ziara yake hiyo, ungana na Joshua Mmali akisimulia katika makala hii..