Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sekta ya biashara ni muhimu katika maendeleo:Ban

Sekta ya biashara ni muhimu katika maendeleo:Ban

Majadiliano ya siku mbili kuhusu sekta ya biashara na umuhimu wake  kuelekea mkutano wa tatu wa kimataifa kuhusu uwezeshaji wa kifedha na maendeleo utakaofanyika mjini Addis Ababa, yameanza leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo Katibu Mkuu Ban Ki- moon amesema sekta binafsi ni muhimu katika utekelezaji wa  malengo ya maendeleo endelevu baada ya 2015.

Ban amewaambia wawakilishi wa mashirika ya kibiashara na wadau wa maendeleo kuwa kuelekea katika mkutano huo uwezeshaji wa kifedha ni muhimu hivyo akasisitiza..

(SAUTI ya Ban)

Dunia inahitaji mkakati thabiti wa kifedha katika kukabiliana na changamoto na kufanikisha maendelo endelevu na jumuishi.

Majadialino hayo hapo kesho yatajikita katika umuhimu wa asasi za kiraia katika uwezeshaji wa kifedha na maendeleo.