Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo maalumu kupitia mtandao kuwapa sauti mamilioni ya wafugaji: FAO

Mfumo maalumu kupitia mtandao kuwapa sauti mamilioni ya wafugaji: FAO

Mfumo maalumu wa kutoa elimu ya ufugaji kupitia mtandao  umezinduliwa leo Jumatatu na shirika la chakula na kilimo duniani FAO na washirika wake.

Kwa mujibu wa FAO kuna mamilioni ya wafugaji  duniani kote ambao wanamiliki ardhi.

Licha ya umuhimu wao katika uzalishaji wa chakula na mfumo wa maisha kwa ujumla ,shughuli za kilimo za wafugaji hao ambao mara nyingi ni wa kuhamahama zinakabiliwa na changamoto nyingi.

Helena Semedo ni Naibu Mkurugenzi Mkuu FAO na anaeleza changamoto zinazowakabili.

(SAUTI YA HELENA SEMEDO)

Uwezo wao wa kuishi katika mazingira magumu, wafugaji wanauwezo wa kuzalisha chakula mahala ambapo mazao hayawezi kupandwa, lakini hata hivyo matakwa yao hayajapewa kipaumbele na serikali na jumuiya ya kimataifa, maisha yao yameathiriwa na kulazimishwa kubadili mfumo wao wa maisha ya kuhama kuhama, kupungua kwa na mgawanyiko wa maeneo ya malisho, na kuvurugwa kwa barabara wanazotumia kuhama hama, na serikali mara nyingi inashindwa kuwapa huduma ya msingi ya afya na elimu.”