Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunahakikisha watoto wa kike wanajitambua: Bi. Maembe

Tunahakikisha watoto wa kike wanajitambua: Bi. Maembe

Tanzania imesema imechukua hatua ili kuhakikisha watoto wa kike wanaoanza darasa la kwanza wanaendelea na masomo hadi wanapohitimu ili kuendeleza mafanikio yaliyopatikana ya uwiano sawa wa uandikishaji watoto wa kike na wa kiume shuleni.

Akihojiwa na Idhaa hii kando mwa vikao vya mkutano wa 59 wa kamisheni ya hali ya wanawake jijini New York, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto Anna Maembe ametaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kuanzisha kwa elimu ya afya shuleni ili mtoto wa kike aweze kujiamini na kuishi ndoto yake.

(Sauti ya Bi. Maembe)

Bi. Maembe amesema tayari wameanza kupitisha maazimio ya kuendeleza baadhi ya mambo ambayo yalikubaliwa Beijing miaka 20 lakini bado hayajafanikiwa ikiwemo mwanamke kuwa na uamuzi kuhusu masuala ya uzazi.

(Sauti ya Bi.Maembe)