Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatuwezi kufanikiwa ipasavyo tukiengua asilimia 50:Ban

Hatuwezi kufanikiwa ipasavyo tukiengua asilimia 50:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema wito wa kuchukua hatua za kutokomeza pengo la usawa wa kijinsia duniani na uwezeshaji wanawake hauwezi kupuuzwa.

Amesema hayo mwishoni mwa mkutano wa kimataifa kuhusu wanawake kwenye uongozi na maamuzi huko Santiago, Chile.

Amesema ari iliyodhihirishwa kwenye mkutano huo ya kutaka kuondoa pengo la usawa, kuondoa vikwazo, kuwekeza kwa wanawake na wasichana na kuachana na maneno sasa iwe vitendo ni lazima sasa izae matunda.

Ban amesema hakuna cha kusema kesho, wakati ni huu kwani dunia haiwezi kufanikisha asilimia 100 ya malengo yake iwapo asilimia 50 ya wakazi wake wanaenguliwa.

Kwa mantiki hiyo amesema ili malengo ya maendeleo endelevu yafanikiwe ni lazima wanawake wawe msingi wa harakati hizo.

Katibu Mkuu amesema Umoja wa Mataifa kwa upande wake utakuwa mstari wa mbele na kila mtu achukue hatua ya kuweka dunia bora na mustakhbali wenye haki sawa kwa wanawake na wanaume.