UNESCO yalaani kifo cha mwanahabari DRC

UNESCO yalaani kifo cha mwanahabari DRC

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO , Irina Bokova, amelaani kuuliwa kwa mwanahabari Chamwami Shalubuto huko Goma,kaskazini mwa Kivu nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC .

Taarifa ya UNESCO imemkariri Bi Bokova akitaka hatua za usalama dhidi ya wanahabari zichukuliwe. Nchini DRC Langi Stany wa radio washirika radio Umoja amehudhuria mazishi ya mwanahabari huyo na kutuandalia ripoti ifuatayo .

(TAARIFA YA LANGI)