Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika kujadili mustakabali wa bara hilo katika mabadiliko ya tabianchi

Afrika kujadili mustakabali wa bara hilo katika mabadiliko ya tabianchi

Wadau wa masuala ya mazingira barani Afrika wanakutana mjini Adis Ababa Ethiopia  kujadili mustakabli wa bara hilo katika makabiliano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi kwa mwaka 2015.

Mkutano huo unaofanyika January 21 hadi 23 unafuatia maazimio ya mkutano wa mazingira nchini Peru  COP 20 ikiwamo ahadi ya zaidi ya dola bilioni kumi za kusaidia kupambana na athari za maabdilio ya tabia nchi.

Miongoni mwa washiriki wa mkutano huo ni  Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira kwenye ofisi ya Makamu wa Rais nchini Tanzania Richard Muyungi ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa kamati ya dunia ya sayansi na teknolojia ya mabadiliko ya tabia nchi

(SAUTI MUYUNGI)