Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua Moustapha Soumaré wa Mali kama naibu wa mjumbe Huko Sudan

UN Photo/Devra Berkowitz
Moustapha Soumare,

Ban amteua Moustapha Soumaré wa Mali kama naibu wa mjumbe Huko Sudan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Moustapha Soumaré raia wa Mali kuwa Naibu Mwakilishi Maalum wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS.

Katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Msemaji wa Katibu Mkuu, Bw Soumaré atachukua nafasi ya Raisedon Zenenga wa Zimbabwe, ambaye atachukua nafasi ya wadhifa wa Naibu Mwakilishi Maalum wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM.

Msemaji wa Bw Ban alimshukuru Bw Zenenga kwa ari na mchango wake bora kwa kazi ya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Sudan Kusini.

Kabla ya uteuzi wake, Soumaré alikuwa Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia UNMIL, 2009-2012.