Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNSMIL yakaribisha kutolewa kwa nakala ya awali ya Katiba ya Libya

UN Photo/Iason Foounten
Picha:

UNSMIL yakaribisha kutolewa kwa nakala ya awali ya Katiba ya Libya

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, UNSMIL umeakaribisha tangazo lilotolewa na Baraza la kuandika katiba nchini humo, CDA ya kutoa ripoti yake ya awali kwa ajili ya majadiliano na maoni ya umma.

Katika taarifa, UNSMIL imesema, japo CDA ilifanya kazi katika mazingira magumu imeonyesha uamuzi wake wa kutoa nakala ya katiba ambayo huonyesha matarajio ya Walibya wote, na kutambua umuhimu wa kuwashirikisha wananchi .

Huku wengi wakiwa na hamu ya kuona Nakala ya mwisho ya katiba haraka iwezekanavyo, ujumbe imefurahishwa na CDA kwa sababu ya majadiliano ya makini , sawa na kuendeleza kazi zake katika muda uliopangwa.

Halikadhalika, UNSMIL imetaja tangu mwanzoni, mchakato huu wa kuandika katiba umebuniwa, kupangwa, na kuongozwa na Walibya na kwa hiyo Umoja wa Mataifa umerejelea ahadi yake ya kuendelea kuisaidia shughuli hiyo kadri CDA inavyoomba