Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa elimu Libya wapatiwa mafunzo ya mitaala

Picha: UNICEF

Wataalamu wa elimu Libya wapatiwa mafunzo ya mitaala

Kiasi cha wataalamu 17 kutoka idara mbalimbali za Wizara ya Elimu ya Libya wamehudhuria mafunzo maalumu yajulikanayo Zarziz yaliyoendeshwa katika Mji Mkuu wa Tunisia, Tunis.

Mafunzo hayo yaliyokuwa ya siku nane yalikuwa yamejikita katika maeneo mbalimbali ikiwamo yale yanayohusu uboreshaji wa mitaala ya elimu.

Kupitiwa upya kwa mitaala ya elimu nchini Libya kunatokana na ukweli wa mambo wa kushuka kiwango cha elimu nchini humo.