Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atangaza mkuu mpya wa UNMEER, ni Ahmed kutoka Mauritania

Ismail Ould Cheikh Ahmed. Picha: OCHA/David Gough

Ban atangaza mkuu mpya wa UNMEER, ni Ahmed kutoka Mauritania

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Ismail Ould Cheikh Ahmed wa Mauritania kuwa mwakilishi wake na mkuu mpya wa ujumbe wa Umoja huo unaohusika na dharura ya Ebola, UNMEER.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imesema Ahmed anachukua nafasi ya Anthony Banbury ambaye atarejea New York mapema mwezi ujao.

Ban amemshukuru Banbury kwa mchango na uongozi wake kwenye harakati dhidi ya Ebola tangu ateuliwe kukabiliana na mlipuko huo mwezi Septemba mwaka huu.

Taarifa hiyo imesema Mkuu huyo mpya wa UNMEER atashirikiana na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ebola Dkt. David Nabarro pamoja na serikali na wadau wengine ili kuendeleza harakati dhidi ya ugonjwa huo.