Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa magharibi mwa Afrika wakutana kujadili ebola

Picha: UNICEF/Liberia/2014

Viongozi wa magharibi mwa Afrika wakutana kujadili ebola

Viongozi wakuu wa nchi za Afrika Magharibi wamekutana kwa siku moja nchini  Liberia ili kuweka mikakati ya kudhibiti homa ya ebola inayoendelea kuliandama eneo hilo. Taarifa kamili na George Njogopa.

(Taarifa ya George)

Wote kwa pamoja wamejadili umuhimu wa kuongeza ushirikiano na wigo wa kupashana habari kwa kuwa hiyo ndiyo muafaka ya kuishinda homa hiyo.

Viongozi waliohudhuria mkutano huo uliofanyika mjini Monrovia ni pamoja na kutoka Sierra Leone, Guinea, Mali na Liberia kwenyewe. Pia mkutano huo ulizijumuisha  nchi jirani za Nigeria, Ivory Coast na Senegal.

Akizungumza kwenye mkutano huo, mwakilishi wa Umoja wa Mataifa anayehusika na kampeni ya kukabiliana na ebola Anthony Banbury aliwahimiza viongozi haa kuendelea kukutana ili kubadilishana ujuzi na taarifa muhimu.