Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UN Maziwa Makuu ataka haki za binadamu zizingatiwe

Said Djinnit.Picha ya UN

Mjumbe wa UN Maziwa Makuu ataka haki za binadamu zizingatiwe

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Maziwa Makuu Said Djinnit amesisitiza umuhimu wa watu kuheshimu haki za binadamu.

Akizungumza mjini Nairobi, Kenya katika kilele cha siku ya haki za binadamu, Djinnit amesema kila binadamu duniani amezaliwa huru hivyo anapaswa kuheshimiwa na kujaliwa utu wake.

Huku akinukuu kipengele kimojawapo kutoka Azimio la Kimataifa Haki za Binadamu Djinnit amesema kuwa serikali zinawajibu wa kuhakikusha zinalinda na kutetea haki za binadamu na wala siyo vinginevyo akigusia mauaji yanayoendelea huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati.