Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vichochezi na harakati dhidi ya maambukizi ya ukimwi

Vichochezi na harakati dhidi ya maambukizi ya ukimwi

Ukimwi ugonjwa ulioanza kutikisa dunia miaka ya 1980 na kusababisha vifo vya maelfu ya watu, sasa angalau kuna nuru kutokana na matibabu dhidi ya magonjwa nyemelezi na hata huduma za upimaji ili watu waweze kufahamu afya zao. Kutokana na umuhimu wa harakati za kutokomeza ugonjwa huo, Umoja wa Mataifa uliamua kuwa kila tarehe Mosi ya mwezi Disemba iwe ni siku ya ukimwi duniani! Siku hii inatoa fursa ya kutathmini kile kilichofanyika, mafanikio yaliyopatikana na changamoto zake! Je hali baada ya zaidi ya miongo mitatu iko vipi?

Basi ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii ya wiki.