Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujuzi wa waandishi ni muhimu katika matangazo ya radio

Ujuzi wa waandishi ni muhimu katika matangazo ya radio

Jumatano ya tarehe 13 mwezi huu wa Februari dunia iliadhimisha siku ya Radio duniani. Siku hii hutoa fursa kwa radio za kimataifa, kitaifa na za kijamii kutathmini shughuli zao za kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha. Mathalani mchango wa Radio katika ukombozi wa kisiasa, kiuchumi na kijamii na hata usalama wa waandishi wa habari. Radio imebuniwa zaidi ya Miaka 100 lakini hadi sasa umuhimu wake unaendelea kubakia ule ule kwa kuzingatia kuwa gharama yake ni nafuu na inaweza kuwafikia watu wengi kwa wakati mmoja. Hata hivyo mengi yanazingatiwa kwa kutambua uwezo huo wa radio.