Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa walaani shambulio hekaluni Jerusalem

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mashariki ya Kati, Robert Serry wakati wa kikao cha Baraza la Usalama.Picha/UM/Loey Felipe

Umoja wa Mataifa walaani shambulio hekaluni Jerusalem

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mchakato wa amani mashariki ya kati Robert Serry ameeleza kuchukizwa na shamblio la asubuhi ya leo katika hekalu mashariki mwa Jerusalem.

Mratibu huyo maalum amesisitiza katika taarifa yake kuwa Umoja wa Mataifa unatoa wito wa dharura kwa pande zote kufanya kila liwezekanalo kuepusha kuendelea kwa hali liyopo ya mvutano Jerusalem.

Amesema anaomboleza pamoja na familia za wahanga wa shambulio hilo.