Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

AMISOM na OCHA wazindua miongozo ya kurahisisha utendaji wao Somalia

Wakati wa uzinduzi.(Picha ya AMISOM)

AMISOM na OCHA wazindua miongozo ya kurahisisha utendaji wao Somalia

Ujumbe wa Afrika nchini Somalia, AMISOM na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA wamezindua miongozo mahususi kwa ajili ya kurahisisha utendaji wa wasaidizi wa kibanadamu na wale wa kijeshi nchini humo.Uzinduzi huo umefanyika mjini Mogadishu ambapo Naibu Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia na Mratibu Mkuu wa Masuala ya kibinadamu Philippe Lazzarini amesema miongozo inalenga kuweka misingi iliyokubaliwa na pande zote zinazoendesha shughuli zao nchini Somalia.

Amesisitiza umuhimu wa AMISOM kuweka mazingira bora ili watoa huduma za kibinadamu waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo akiongeza kuwa miongozo ya aina hiyo ni muhimu kuhakikisha kuna uhusiano mzuri baina ya watendaji na wakati huo huo msaada unawafikia