Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ustawi wa mwanamke Afrika Mashariki ni changamoto, wataka serikali iwekeze vijijini

Wanawake wa kijijini licha ya mchango wao kwenye jamii bado mahitaji yao hayapatiwi kipaumbele. (Picha:UN /Albert González Farran)

Ustawi wa mwanamke Afrika Mashariki ni changamoto, wataka serikali iwekeze vijijini

Mwanamke wa kijijini! Huyu huchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya jamii yake, taifa na hata dunia kwa ujumla kupitia shughuli mbalimbali anazozifanya.Iwe ni kilimo, ufugaji, kulea familia yake na hata kuleta uzao au nguvukazi duniani. Hata hivyo yeye hukumbana na changamoto kadhaa ikiwamo ukatili na mengineyo hiyo ni kauli ya Umoja wa Mataifa kwa siku ya kimataifa ya mwanamke wa kijijini ambayo huadhimishwa Oktoba 15 kila mwaka kuanzia mwaka 2008.

Je hali ikoje? Ungana na Grace Kaneiya kwenye makala hii ya wiki.