Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfanyakazi mwingine wa Umoja wa Mataifa augua Ebola Liberia

UN Photo/Andrey Tsarkov
Askari wa kulinda amani wa UNMIL wamevaa barakoa wakiwa kazini kwenye ofisi ya umoja wa mataifa, Monrovia, Liberia. Picha:

Mfanyakazi mwingine wa Umoja wa Mataifa augua Ebola Liberia

Mfanyakazi mmoja wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia, UNMIL ameripotiwa kuugua Ebola, akiwa ni mfanyakazi wa pili wa Umoja wa Mataifa kuambukizwa ugonjwa huo nchini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema kwamba mkuu wa UNMIL, Karin Landgren ametoa taarifa hiyo jumatano tarehe 8 Oktoba, akieleza kwamba UNMIL imechukua hatua zote zinazohitajika ili kuzuia maambukizi mengine.

Amesema hivi sasa watu wote ambao wamekuwa karibu na mfanyakazi huyo akiwa mgonjwa wanapimwa na kuwekwa chini ya karantini, na makazi yao yamesafishwa na dawa maalum ili kuondoa virusi vya Ebola, kulingana na taratibu za Shirika la Afya Duniani, WHO.

Mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa aliyekuwa ameathirika na Ebola alifariki dunia tarehe 25 Septemba.