Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yawezesha ustawi wa wakimbizi Burundi

UNHCR yawezesha ustawi wa wakimbizi Burundi

Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi nchini Burundi kwa kushirikiana na serikali ya nchi hiyo linasaidia ustawi wa wakimbizi wanaorejea nchini humo kutoka nchi mbalimbali wengi wao wakiwa ni kutoka Tanzania.

Katika mahojiano na idhaa hii Mwakilishi mkazi wa UNHCR nchini Burundi Abel Mbilinyi amesema shirika hilo linawajengea makazi na kusaidia kuendeleza wale wenye ujuzi na waliokuwa wanafanya kazi mbalimbali katika makambi.

(SAUTI MBILINYI)

Hata hivyo amesema UNHCR inakabiliana na changamoto kubwa ya lundo la wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo DRC ambapo mwaka huu pekee takribani wakimbizi elfu tano wampokelewa.