Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu lajadili operesheni za kijeshi kukabili ugaidi

UN Photo/Sylvain Liechti
Drones.

Baraza la haki za binadamu lajadili operesheni za kijeshi kukabili ugaidi

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limekuwa na majadiliano yaliyolenga kukabiliana na vitendo vya ugaidi vinavyoendelea kujitokeza katika maeneo mbalimbali.

Katika majadiliano hayo wajumbe kwenye baraza hili wameelezea kuridhishwa kwao na utumiaji wa vifaa vya kijeshi ikiwamo ndege zisizotumia rubani kwa ajili ya kukabiliana na vitendo hivyo vya kigaidi.

Baraza hilo limeunga mkono matumizi ya vifaa hivyo lakini kwa kusisitiza kuwa lazima mashambulizi yoyote yatayofanywa yaambatane na sheria za kimataifa.

Majadiliano hayo yaliongozwa na Dapo Akande

kutoka chuo kikuu Oxford.