Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Changamoto za mabadiliko ya tabianchi katika jimbo la Turkana

Picha ya UNDP - Kenya

Changamoto za mabadiliko ya tabianchi katika jimbo la Turkana

Nchini Kenya, katika jimbo la Turkana, watu wa asili wanakumbwa na matatizo mengi yaliyosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Ukosefu wa maji umeathiri uandikishwaji shuleni kiasi kwamba serikali ya Kenya, kwa ufadhili kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP, imeamua kujenga matangi ya maji shuleni.

Kwa maelezo zaidi, ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.