Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WMO yaonya kuhusu ongezeko hewa ukaa

UNEP(UN News Centre)
Photo: UNEP(UN News Centre)

WMO yaonya kuhusu ongezeko hewa ukaa

Shirika la hali ya hewa  duniani, WMO limesema kiwango cha hewa ukaa inayosambaa angani katika kipindi cha mwaka 2013 kilikuwa cha juu zaidi kuwahi kushuhudiwa duniani jambo ambalo linatoa tahadhari ya kufanyika jambo la dharura kunusuru hali hiyo. Taarifa kamili na George Njogopa.

(Taarifa ya George)

Katika jarida lake la nyumba zinazojali mazingira, shirika hilo limesema kuwa kiwango cha miaka kilichorekodiwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 2013 kilifikiwa wastani wa asilimia 34.

Limesema kiasi hicho ni kikubwa mno mpaka kusababisha mabadiliko ya tabia nchi kutokana na uzalishaji wa wingi wa gesi ukaaa yaani Carbondioxide.

Takwimu zilizotolewa na shirika hilo zinaonyesha kuwa kiwango cha uzalishaji wa hewa ukaa kiliongezeka zaidi katika mwaka 2012 na mwaka uliofuata, kikiwa ni kikubwa zaidi tangu kile kilichoshuhudiwa mwaka 1998.

Katibu Mkuu wa shirika hilo Michel Jarraud amesema kuwa kutolewa kwa takwimu hizo kunaakisi hali halisi ya mwenendo wa dunia ambayo inakabiliwa na mabadiliko ya tabia nchi kutokana na shughuli za kila siku za binadamu.

(Sauti ya Michel Jarraud )

"Bado inawezekana kuchukua hatua, lakini tutahitaji uamuzi wa ujasiri. Hatuna muda, na kadri tunavyozidi kusubiri, ndivyo itakavyokuwa vigumu zaidi, ghali zaidi, na yenye changamoto kubwa zaidi”