Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yalaani mauaji ya mwanahabari wa Marekani, Steven Sotloff

UNESCO yalaani mauaji ya mwanahabari wa Marekani, Steven Sotloff

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Irina Bokova, ameeleza kushangazwa na mauaji ya mwanahabari wa Marekani, Steven Sotloff, na ktoa wito kwa makundi ya wapiganaji nchini Syria kuwaachia huru mara moja mateka wa kiraia.

Bi Bokova amelaani vikali mauaji ya Steven Sotloff, akisema kuwa kama mwenzie James Foley aliyengulia kuuawa, Sotloff alikuwa mtu jasiri aliyefanya kazi kama mwandishi wa habari, akijikita kuuambia ulimwengu kinachoendelea kwenye maeneo ya matukio.

Mkurugenzi huyo wa UNESCO amesema inasikitisha kuwa wanataaluma hawa jasiri wanaopewa msukumo na hamu ya kutambua ni vipi watu wanaathiriwa na vita na kuusimulia ulimwengu hadithi zao wanakabiliwa na ukatili kama huo.

Ametuma risala za rambi rambi kwa familia na marafiki wa Steven Sotloff, na kuzitaka serikali kuimarisha usalama wa wanahabari kwa kuhakikisha kuwa wanaotenda ukatili kama huo wanawajibishwa kisheria.