Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumuiya ya kimataifa lazima isaidie harakati za SIDS za mabadiliko:Ban

Katibu Mkuu wa UM akizungumza wakati wa mkutano wa Tatu wa SIDS huko Apia, Samoa. (Picha-UM)

Jumuiya ya kimataifa lazima isaidie harakati za SIDS za mabadiliko:Ban

Jumuiya ya kimataifa ina dhima muhimu katika kuhakikisha nchi za visiwa vidogo zinazoendelea zinasaidiwa ili harakati zao maendeleo endelevu na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ziweze kuzaa matunda.

Ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon aliyoitoa huko Apia, Samoa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa tatu wa nchi za visiwa vidogo zinazoendelea SIDS, mkutano ulioanza Jumatatu kwa saa za Samoa.

Ban amesema kwa kushughulikia masuala yanayokumba nchi za visiwani, maendeleo endelevu yanaweza kupatikana duniani kote,

 (Sauti ya Ban)

"Mjumuiko huu wa mataifa haya ya visiwa tunaoita SIDS wanakabiliwa na mabadiliko ya tabia nchi na suala la maendeleo endelevu. Jukumu letu ni kuhakikisha SIDS ziko mstari wa mbele kuanzisha majibu ambayo ulimwengu mzima unahitaji.”

Mkutano wa Samoa unafanyika kabla ya mkutano wa viongozi kuhusu mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika New York, tarehe 23 mwezi Septemba ambapo nchi za visiwa zinaonekana ziko hatarini zaidi kutokana na ongezeko la viwango vya joto linalofanya kiwango cha maji ya bahari pia kuongezeka.