Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Naweka matumaini kwenye nyaraka iliyopitishwa SIDS: Ban

UN Photo/Evan Schneider
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon(kushoto) na Waziri Mkuu wa New Zealand John Key (kulia). Picha:

Naweka matumaini kwenye nyaraka iliyopitishwa SIDS: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon yuko nchini New Zealand ambako katika mkutano wake na waandishi wa habari amesema ni matumaini yake kuwa nchi hiyo itashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa nyaraka iliyopitishwa kwenye mkutano wa nchi za visiwa vidogo vinavyoendelea SIDS.

Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa New Zealand John Key ambapo Ban amesema nchi hiyo kama vilivyo visiwa vingine vidogo vinakumbwa na mabadiliko ya tabianchi.

Amesaema changamoto zinazokumba maeneo hayo kama vile biashara ya kimataifa na usafirishaji zinaweza kupatiwa suluhu kwa njia ya ushirikiano thabiti kutoka jamii ya kimataifa. Hivyo akasema..

Ameongeza kuwa jambo muhimu ni nyaraka ya SAMOA iliyopitishwa na mkutano wa SIDS itekelezwe. Nimewahakikishia kuwa hiyo nyaraka itaungwa mkono na kutumika kwenye majadiliano yanayoendelea ya maandalizi ya ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015. Hilo ndilo tunapaswa kufanya na nimepata hakikisho kutoka kwa Waziri Mkuu Key na serikali yake kuwa wataunga mkono.

Akiwa New Zealand Ban anatembelea miradi ya kilimo endelevu an uzalishaji nishati isiyo na madhara kwa mazingira.