Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa SIDS wakamilika, wadau waahidi fedha kuwezesha nchi za visiwa vidogo

Picha: SIDS

Mkutano wa SIDS wakamilika, wadau waahidi fedha kuwezesha nchi za visiwa vidogo

Mkutano wa nchi za visiwa vidogo zinazoendela SIDS umemalizika  leo nchini Samoa kwa ahadi ya michango ya zaidi ya dola bilioni 1 ili kusaidia visiwa hivyo kukabiliana na athari za  mabadiliko ya tabianchi.

Wakati mkutano huo ukiwa umekamilika washiriki wameanza kile kinachojulikana kama "mzunguruko wa ngoma yenye wito  wa utekelezaji" yaani "drum roll of action" kabla ya mkutano wa kilele hapa New York baadaye mwezi huu ambapo katibu wa mkutano huo Wu Hongbo amesema mikakati iliyotangazwa ni fursa ya kusongesha uhusishaji wa nishati, uzuiaji wa majanga na upatikanaji endelevu wa chakula.

Akizungumzia umuhimu wa mkutano huo wa Samoa uliofikia kilele, mtaalamu wa masula ya mazingira ambaye ni mkurugenzi wa mazingira ofisi ya makamu wa Rais Tanzania Julius Ningu anasema..

(SAUTI NINGU)