Wajumbe wa Baraza la usalama wataka uwajibikaji kwa mzozo Sudan Kusini
Normal
0
false
false
false
MicrosoftInternetExplorer4
st1\:*{behavior:url(#ieooui) }
/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:"Table Normal";
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-parent:"";
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin:0in;
mso-para-margin-bottom:.0001pt;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:10.0pt;
font-family:"Times New Roman";
mso-ansi-language:#0400;
mso-fareast-language:#0400;
mso-bidi-language:#0400;}
Wajumbe wa baraza la usalama waliopatiwa fursa ya kuchangia hoja baada ya kuwasilishwa kwa ripoti kuhusu hali ya haki za binadamu Sudan Kusini wamesema kinachoendelea hakikubaliki na ni aibu kubwa.
Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe Sudan Kusini yalianza tarehe 15 Disemba mwaka jana kati ya vikosi vya serikali na vile vinavyomuunga mkono Makamu Rais wa zamani Riek Machar.
Mmoja wa wajumbe hao ni Mwakilishi wa kudumu wa Rwanda kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Eugene Richard Gasana ambaye amesema matumaini yaliibuka wakati wa uhuru wa Sudan Kusini mwaka 2011..
(Sauti ya Balozi Gasana.)
“Hata hivyo miaka mitatu baadaye na kwa kuzingatia kuenea kwa mauaji ya raia pamoja na hali ya haki za binadamu kama ilivyoelezwa na watoa ripoti wa leo na pia kusisitizwa na Balozi Samantha, hatuwezi kubakia watazamaji tu. Huwezi kugombania uhuru kwa miaka na baadaye kugeuka na kuanza kuua raia wako wewe mwenyewe. Ni aibu!”
Mwakilishi wa Kudumu wa Uingereza Balozi Mark Lyall Grant akasema ripoti za Bi. Navi Pillay na Adama Dieng zimeweka dhahiri ukiukwaji wa haki za binadamu na akaunga mkono hatua za Muungano wa Afrika na IGAD za kupatia suluhisho la mapigano yanayoendelea. Balozi akatoa mapendekezo.
(Sauti ya Balozi Grant)
“Kwanza lazima tukomeshe ukwepaji sheria. Uwajibikaji na haki ni muhimu kwa maridhiano ya kitaifa. Tuhuma za ukiukwaji wa haki na ukatili ni lazima zichunguzwe bila upendeleo na wahusika wachukuliwe hatua. Tunapongeza hatua za tume ya uchunguzi iliyoundwa na Muungano wa AFrika. Lakini wakati jitihada hizo zikiendelea itakuwa vyema kwa OHCR kuweka bayana mienendo yoyote ya ukiukwaji wa haki kwa ajili ya uwajibikaji Sudan Kusini. Halikadhalika tunaomba OHCR kufikiria uchunguzi wa kina kwa matukio ya hivi karibuni ya kikatili huko Bentiu”.