Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiwango cha mauaji ya visasi Sudan Kusini na ubinafsi wa viongozi vyatisha: Pillay

Wajumbe wa Baraza la Usalama.(Picha UM//Paulo Filgueiras)

Kiwango cha mauaji ya visasi Sudan Kusini na ubinafsi wa viongozi vyatisha: Pillay

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limepatiwa muhtasari wa ziara iliyofanywa na viongozi waandamizi wa umoja huo Sudan Kusini ambapo wamejulishwa kuwa kinachoendelea sasa ni mauaji ya visasi na yanazidi kutishia wananchi ambao sasa wamejawa na hofu.

Navi Pillay, Kamishna Mkuu wa Haki za binadamu alisema visasi viko dhahiri na raia hata waliosaka hifadhi ndani ya maeneo ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS wana hofu na wanasema wanahisi wakihamishwa watakuwa salama zaidi.

Bi. Pillay amesema visasi vilikuwa dhahiri ..

(Sauti ya Pillay)

“Hata hivi karibuni, gavana wa jimbo la Lakes aliwaeleza mkusanyiko wa vijana mwishoni mwa wiki na namnukuuu ‘kile tunachofanya sasa ni kulipiza kisasi. Ukinifinya, nakufinya! Hakuna kusameheana, iwapo mtu atakufinya mara kwa mara na hufanyi hivi, unaonyesha dalili ya udhaifu”

Hata hivyo amesema ni vyema taasisi za mahakama Sudan Kusini zikaimarishwa ili kuwajibisha wahusika na amekumbusha Baraza kuwa wananchi wake wanatarajia chombo hicho kutumia uwezo wake kuwaondolea machungu.

(Sauti ya Pillay)

“Ni hatua ya wazi na ya uamuzi  ya kuweka uwajibikaji ndiyo itaweza kusaidia kusitisha wimbi la mauaji ya visasi na kurejesha hisia ya mustakhabali wa pamoja nchini kote.”

Naye Adama Dieng Mshauri wa Katibu Mkuu kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari akaikita hotuba yake kwenye maeneo yenye viashiria vya mauaji ya kimbari akitolea mfano tukio moja la radio  huko Bentiu kutumika kutangaza ushawishi dhidi ya wafuasi wa serikali.

(Sauti ya Dieng)

“Iliripotiwa kuwa huko Bentiu wapiganaji wafuasi wa Riek Machar walichochea raia kushambulia watu wa kabila la Dinka hata kushawishi wasaidie kufanya ukatili wa kingono dhidi ya mwanamke. Hii haikubaliki kabisa.”

Bwana Dieng akaeleza jukumu la serikali..

(Sauti ya Dieng)

“Serikali ni lazima ikubali kuwa ina wajibu wa kimsingi wa kulinda raia wote wa Sudan Kusini bila kujali utaifa, makabila yao, au mrengo wa kisiasa, na ipatie kipaumbele jukumu hilo. Kurushia lawama kundi moja au jingine ni kutokuwajibika na ni hatari kubwa.”

Dieng na Pillay wamesifu kazi inayofanywa na UNMISS tena katika mazingira magumu wataka ujumbe huo uimarishwe kwa watendaji ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi wanapolinda raia.