Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwepo wa wanawake kwenye vikao huleta mabadiliko: Bi. Santos Pais

Uwepo wa wanawake kwenye vikao huleta mabadiliko: Bi. Santos Pais

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika kupinga ukatili dhidi ya watoto Marta Santos Pais amesema amekuwa akitumia fursa ya uwepo wake ndani ya Umoja huo kuchagiza hatua za mabadiliko stahili kwa maisha ya watoto wa kike na wa kiume wanaokumbwa na madhila sehemu mbali mbali duniani.

Amesema hayo wakati wa mahojiano maalum na watoto kuhusu siku ya wanawake duniani akieleza kuwa fursa ya kushuhudia maisha halisi ya watoto humwezesha kuchangia kwa kina kwenye vikao husika ndani ya chombo hicho kikubwa zaidi duniani.

(Sauti ya Marta)

Nafikiri kwa kuwa mwanamke kunatuwezesha kuonyesha nini tofauti ya kile tunachojadili kuhusu maisha ya mtoto wa kike au kiume niliyekutana naye Thailand, anayeishi Tanzania, Afrika au watoto wa kike huko Uingereza. Na kwa kuleta hisia hiyo nafikiri wanawake wanasaidia kuchochea suluhu inayoweza kuleta tofauti, na tofauti si tu ubora kupindukia kama unavyosema insha ya shule imekuwa bora sana! Bali wanaweka mtazamo ambao ni aghalabu kuupata.”

Bi. Pais amesema kuwa mwanamke ndani ya chombo hicho kunampatia fursa ya kuweza kushawishi wanaume na hata wavulana kushiriki katika kupitisha uamuzi ambao unakuwa bora zaidi kwa maslahi ya jamii yote.