Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lasifu makubaliano ya Sudan Kusini, lataka utekelezaji wa dhati

Baraza la usalama lasifu makubaliano ya Sudan Kusini, lataka utekelezaji wa dhati

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wameunga mkono hatua ya hivi karibuni zaidi ya pande mbili kinzani huko Sudan Kusini kutia saini mjiniAddis AbabaEthiopiamakubaliano ya kusitisha mapigano.

Katika taarifa yao wametaka pande husika ambazo ni serikali na wafuasi wanaomuunga mkono makamu wa Rais wa zamani, kutekeleza kwa dhati kama hatua ya awali ya mchakato wa kuleta amani ya kudumu nchini humo na pia kupatia suluhu la kudumu chanzo cha mgogoro huo.

Wajumbe wamesema mchakato shirikishi wa kisiasa, maridhiano ya kitaifa na uanzishaji wa taasisi thabiti za umma ni mojawapo ya njia ya kuleta amani ya kudumu.

Wajumbe pia wameunga mkono jitihada za usuluhishi zinazoongozwa na IGAD na wabia wake za kuharakisha suala la kuachiwa kwa wafungwa wa kisiasa na kuhakikisha wanashiriki kwenye mchakato wa maana wa kisiasa nchini humo.