Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila kupunguza kiwango cha joto, maendeleo endelevu ni ndoto: Ban

Bila kupunguza kiwango cha joto, maendeleo endelevu ni ndoto: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amehutubia kongamano la dunia kuhusu uchumi huko Davos Uswisi na kuonya kuwa bila kupunguza kiwango cha joto duniani, harakati za kutokomeza umaskini na kufikia maendeleo endelevu zitakabakia ndoto. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Bwana Ban ametumia maudhui ya kongamanohilokuhusu hali ya hewa, ukuaji na maendeleo na kuweka bayana kuwa kitisho cha mabadiliko ya tabianchi ni dhahiri na ameshuhudia Ufilipino, Ukanda wa Sahel na hataKiribati. Amesema athari zake zinakumba dunia nzima kuanzia jamii, sekta ya biashara iwe kubwa au ndogo na hata kutishia usalama wa mataifa. Amesema fikra kuwa harakati za kudhibiti mabadiliko ya tabianchi zinakwamisha ukuaji uchumi hazina msingi wowote.

 “Kudhibiti mabadiliko ya tabianchi kutatuweka sote kwenye mwelekeo wa kufikia malengo endelevu ya maendeleo. Na kuendesha shughuli zetu za biashara kiendelevu zaidi kutatusaidia kushughulikia mabadiliko ya tabianchi. Hivyo basi  mambo haya mawili yanaimarishana kwa pamoja na yanasaidiana.

Katibu Mkuu amerejelea mkutano wa ngazi ya juu kuhusu mabadiliko ya tabianchi atakaouitisha mjiniNew York mwezi Septemba mwaka huu akisema kuwa ni fursa ya kuweka malengo makuba ya kupunguza utoaji gesi chafuzi na kuimarisha ustahimilivu pindi mabadiliko hayo yanapotokea.

Amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa sekta ya umma na ile binafsi katika kuchochea ubia wa kuwekeza kwenye miradi isiyoharibu mazingira na wakati huo huo kuchochea uchumi